heri ya sikukuu ya krismas wadau woote wa Mtaa Kwa Mtaa Blog

December 25, 2011 Leave a comment
Categories: Uncategorized

Mahafali ya Saba ya Chuo kikuu cha Taifa SUZA yafanyika leo Zanzibar

December 24, 2011 Leave a comment
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA,Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo hicho (hawapo pichani) kabla ya kuwatunuku shahada zao katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohamed Shein,akimtunuku Shahada ya heshima ya chuo kikuu cha Taifa cha SUZA Rais Mstaafu wa
Zanzibar Dr Amani Abeid Karume,wakati wa mahafali ya 7 yaliyofanyika katika viwanja vya chuo Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi Said Salum Bakhresa,kwa mchango wakemkubwa kukisaidia
Chuo,wakati wa mahafali ya 7 yaliyofanyika katika viwanja vya chuo Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha SUZA,Simai Mohamed (kushoto)na Mfanya biashara maarufu Said Bakhresa na Dr Nariman Jidawi,walipompongeza kwa kupata zawadi kutokana na mchango wake mkubwa kwa SUZA,wakati wa mahafali ya 7 chuoni hapo.
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA wakisubiri kutunukiwa Shahada zao na Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wa katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SUZA pamoja na wahitimu wa Chuo ngazi ya Stashahada baada ya kuwatunuku Stashahada zao katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.picha na Ramadhan Othman IKULU ZANZIBAR.
Categories: Uncategorized

ZIARA YA MH. BENDERA , WILAYANI ULANGA , KUANGALIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KWENYE BONDE LA KILOMBERO

December 24, 2011 Leave a comment
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera akionesha mpaka kati ya Kijiji cha Igawa, Malinyi na Pori Tengefu la Bonde la Kilombero, ambapo wananchi wamevamia kwa kulima na kufanya malisho ya mifugo yao.
Diwani wa Kata ya Malinyi , Said Tira wa Chadema ( kulia) akieleza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera ( kati) huku Diwani mwenzake wa CCM Kata ya Igawa,Severus Kamguna, akisikiliza kwa makini
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera, (mwenye miwani) akifuata nyayo za RPC Adolfina Chialo aliyeongoza mstari, kwenda kuangalia uharibifu wa Bonde la Kilombero.
Mifugo nayo ndani ya Pori Tengefu la Bonde la Kilombero
Makazi ya jamii ya wasukuma ndani ya Pori Tengefu, Bonde la Kilombero
Gari la Polisi , Wilaya ya Ulanga, likiwa limenasa kwenye tope , ndani ya mashamba yaliyolimwa katika Bonde la Kilombero.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Igawa, Tarafa ya Malinyi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (hayupo pichani), wakati alipotoa amri ya kuzuia shunghuli za kilimo na ufugaji katika bonde la Kilombero.
Baadhi ya wakulima wa Wilaya ya Ulanga waliovamia bonde la Kilombero , wakirejea baada ya kupata maekelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera ( hayupo pichani).
Baadhi ya wakulima na wafugaji wa jamii ya kisukuma, wakitoka mashambani ili kumsikiliza Mh. Bendera (hayupo pichani).
Sehemu ya Mashamba makubwa yaliyilimwa ndani ya Pori Tengefu katika Bonde la Kilombero, eneo la Maguba, Malinyi , Wilaya ya Ulanga.Picha na John Nditi.
Categories: Uncategorized

misaada mbalimbali yaendelea kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwasaidia waliofikwa na janga la mafuriko

December 24, 2011 Leave a comment
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya misaada iliyotolea na Umoja wa Masheikh na Wanazuoni wa Nchini Tanzania wenye jumla ya thamani ya sh. Milioni 12,kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo,Sheikh Hamis Mataka (mwenye kanzu nyeusi) leo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.Wengine pichani ni wajumbe wa Umoja huo wa Masheikh.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Masheikh na Wanazuoni Nchini,Sheikh Hamis Mataka (katikati) akisoma taarifa fupi ya misaada mbali mbali iliyotolewa na umoja huo kwa ajili ya waathirika wa janga la Mafuriko lililolikumba jiji la Dar es Salaam hivi karibuni wakati walipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (wa pili kulia) leo kwa ajili ya kukabidhi msaada huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq akitoa shukrani kwa wale woote waliofika ofisini kwake leo kwa lengo la kuwasilisha midaada mbalimbali kwa ajili wa waathirika wa Mafuriko yaliyotokea hivi karibu jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kulia) akipokea Misaada ya vyakula kutoka kwa vijana wanaounda Muungano wa Mashirika ya Vijana nchini,Kushoto ni Kiongozi wa Muundano huo,Nyakia Ally na Katikati ni Mjumbe wa Muungano huo,Sostenes Mitti.
Kiongozi wa Muungano wa Mashirika ya Vijana nchini,Nyakia Ally (kushoto) akiongea na vyombo vya habari wakati wa kukabidhi sehemu ya misaada kwa ajili ya waathirika wa Mafuriko jijini Dar es Salaam wakati walipofika kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kulia) kukabidhi misaada yao hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa ya Meneja Mauzo wa DarBrew LTD ambao ni Watengenezaji wa Kinywaji cha Chibuku,Urban Shayo wakati walipofika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kukabidhi Msaada wao kwa waathirika wa Mafuko.
Categories: Uncategorized

POLISI MKOA MJINI MAGHARIBI ZANZIBAR WATAJWA KULETA MAFANIKIO KATIKA HUDUMIA YA MWANAMKE NA MTOTO

December 23, 2011 Leave a comment
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zainzibar imesema mpango wa kuanzishwa kwa dawati linaloshughulikia kesi za kijinsia kwenye vituo vya Polisi hapa nchini kumeongeza uhuru zaidi wa kujieleza kwa watu wanaodhalilishwa na kufika Polisi kuomba huduma za kisheria.

Mkurugenzi wa Idara ya Ustawa wa Jamii, Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar Bi. Halima Khamis, ameyasema hayo wakati alipotembelea Ofisi za Dawati la Polisi mkoa wa Mjini Mgharibi Zanzibar ambapo aliwaongoza wageni kutoka mashirika ya mbalimbali ya Kimataifa kuja kuona mafanikio yaliyopatikana katika ofisi za Dawati hilo.

Mkurugenzi huyo amesema tangu kuanzishwa kwa Dawati hilo katika mkoa wa Mjini Magharibi, Idara ya Ustawi wa Jamii Visiwani Zanzibar imekuwa ikipata ushirikiano mkubwa katika kupata ufumbuzi wa kesi za ukatili wa kijinsia.

Bi Halima amesema uwezo wa kiutendaji unaonyeshwa na Askari walipo kwenye ofisi za Dawati la Wanawake na Watoto mkoa wa Mjini Magharibi, umesaidia kuiwezesha jamii kupata huduma bora na kwa wakati jambo ambalo amesema limechangia kuamsha ari za mapambono dhidi ya matendo ya kikatili kwa wanaweke na watoto Visiwani hapa.

Amesema Ofisi hizo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wageni mbalimbali wa Kimataifa wanaotembelea Visiwani Zanzibar wakitaka kutembelea pia katika ofisi hizo kwa nia ya kujifunza zaidi.

Wakati wa Mkutano wao, Mratibu Msaidizi wa Dawati hilo Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Inspekta Fakih Yusufu Mohammed, aliwaambia wageni hao kuwa, pamoja na changamoto zilizopo, lakini Dawati hilo limepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwezi Aprili mwaka jana (2010).

Inspekta Fakih amesema kuwa umuhimu wa Dawati hilo umefahamika baada ya watu mbalimbali kupatiwa huduma na elimu juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili wa kijinsia.

Amesema hivi sasa idadi ya watu wanaofuata huduma za kisheria katika ofisi za Dawati imeongezeka kutoka watu 11 wa mwaka jana lilipoanzishwa mwaka jana hadi kufikia watu 55 mwaka huu wa 2011.

Ameyataja mafanikio mengine yaliyopatikana kuwa ni pamoja na kutoa mwamko kwa wananchi wanaopatwa na matatizo ya unyanyasaji kijinsia kujitokeza kutoa taarifa Polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe .

Amesema siku za nyuma matatizo kama hayo yalikuwa yakimalizwa katika ngazi ya familia tofauti na sasa ambapo mtazamo huo umebadilika kutokana na elimu inayotolewa juu ya madhara yatokanayo na matendo kama hayo siku za usoni.

Awali akizungumza na ujumbe huo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wajitokeze kutoa kutoa taarofa Polisi na kwenda Mahakamani kutoa ushahidi pale wanaposhuhudia vitendo vya udhalilishwaji wa kijinsia kwa mwanamke na watoto.

Kamanda Aziz amesema kuwa matendo mengi ya kikatili yanafanywa na watu wa familia moja na hivyo kuwafanya watendewa wa makosa hayo na mashahidi kutochukua hatu kwa kuhofia kuwa wakijulikana wataweza kukamatwa na kufikishwa mahakamani na hata kufungwa jela.

Katika ziara hiyo, Bi. Halima alifuatana na wageni kutoka Shirika la Midaasa la Marekani USAID, Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Afya za Familia FHI na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.
Categories: Uncategorized

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWATEMBELEA WANANCHI WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO DAR

December 23, 2011 Leave a comment
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya wananchi waliohifadhiwa katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia majuzi, wakati Makamu alipofika katika Kambi hiyo leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini kuanzia majuzi, wakati makamu alipotembelea katika Kambi ya Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika wa mafuriko hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha jijini kuanzia majuzi. Makamu alifanya ziara hiyo ya kutembelea baadhi ya kambi za waathirika leo Desemba 23.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick (kulia), wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo Jangwani leo Desemba 23. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
Categories: Uncategorized

VODACOM YAWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAAFA YA DAR

December 23, 2011 Leave a comment
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadiq Meck Sadick ksuhoto akiwa na Mbunge wa Kinondoni Bw. Iddi Azan akipokea magodoro kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule .Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Vodacom Bi. Najengwa Mbagga. Vodacom imekabidhi magodoro 430, mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 30 milioni kusaidia kambi za waathirika wa maafa ya Dar es salaam.
Sehemu ya shehena ya magodoro 430 yaliyotolewa msaada na Vodacom kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam yakiwa tayari kukabdhiwa kwa kamati ya maafa ya mkoa wa Dar es salaam. Mbali na magodoro Vodacom ilikabidhi pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakishusha sehemu ya magodoro 430 yaliyotolewa na kampuni hiyo katika kambi ya waathirika wa maafa ya Dar es salaam ya Mchikichini. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.
Sehemu ya watoto wanaoishi katika kambi ya waathirika ya maafa ya Dar es salaam katika kambi ya shule ya msingi Mchikichini wakiwa na magodoro yaliyogawiwa na Vodacom kwa waathirika wanaoishi katika kambi hiyo. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii – Vodacom Foundation.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Bi. Beatrice Makangara kushoto na Bi. Jacqueline Tarimo wakiwaongoza wenzao kuelekea kugawa magodoro 430 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom leo imekabidhi msaada wenye thamani ya shilingi 30 Milioni kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam wanaoishi katika makambi maalum yaliyofunguliwa kuwawezesha kujihifadhi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya.

Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa kusaidia jamii – Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule amekabidhi msaada huo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadik Meck Sadiq ukijumuisha magodoro 430 mablanket 800,na vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni kumi.

“Tumeshtushwa sana na hali halisi ya maafa yaliyotukumba jijini Dra es salaam, tumefika hapa kuendeleza utamaduni wa Vodacom kwa kuonesha upendo na kuwa karibu na wananchi katika nyakati za raha na shida.”Alisema Mwakifulefule.

Vodacom imekabidhi msaada huo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ambao umekuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za maendeleo katika jamii na pia kufariji waathirika nyakati za maafa.

“Mafuriko haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi kuwahi kutokea Dar es salaam katika muda wa miaka mingi iliyopita na hivyo ni wazi athari zake ni kubwa, tunatoa pole kwa wote waliopoteza watoto, ndugu na jamaa na wale walionusurika tunawatakia afya njema na faraja katika wakati huu mgumu wa maisha wanaoupitia”Aliongeza Mwakifulefule.

Adha kampuni hiyo imetangaza pia fursa kwa wateja wake na wa wananchi kwa ujumla kuungana na Menejimenti na wafanyakazi wake kuchangia walichonacho kupitia nambari maalum ya maafa ya Vodacom Red Alert na kwa njia ya m-pesa.

Kupitia nambari ya Red Alert wananchi wanaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS wenye neno “MAAFA” kwenda nambari15599 na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.

“Mahitaji kwa wenzetu waliothirika ni makubwa. Tuna imani kuwa wote kwa pamoja tutaonesha umoja, upendo na mshikamano wetu wa kitaifa unaojenga tunu ya Utanzania wetu kusaidia wenzetu ambao kwa wakati huu wapo katika mashaka makubwa wakihitaji faraja ya kila aina”. Amesema Mwakifulefule.

Michango yote itakayokusanywa kupitia nambari hizi itawasilishwa kwa kamati ya Maafa ya mkoa kuongeza nguvu katika juhudi za kuwasaidia waathirika na kwamba utaratibu wa kuwapatia taarifa wachangiaji utakuwepo.

Aidha kampuni ya Vodacom Tanzania imevipongeza kipekee vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa juhudi kubwa za uokozi kwa kushirikiana na wananchi hatua ambayo imesaidia kunusuru maisha ya maelfu ya watu.

Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa

*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.
Hatua ya 2: Chagua 4 – Lipa Bili
Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni – weka namba 155990
Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu – weka namba yako ya simu
Hatua ya 5: Weka kiasi – ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea
Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri
Hatua ya 7:Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia.
Categories: Uncategorized

Ziara ya Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara wa Nishati na Madini kwenye maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko jijini Dar es Salaam

December 23, 2011 Leave a comment
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Eliakim C. Maswi akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wakazi wa eneo la Mbagala Kingugi mara baada ya kutembelea eneo hilo kwa ajili ya kujionea uharibifu wa miundombinu ya umeme uliosababishwa na mafuriko yaliyotokea tangu juzi. Aidha aliambatana na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Eng. William Mhando pamoja na wataalamu kutoka katika shirika hilo na makao makuu ya Wizara ya Nishati na Madini.
Msikiti wa Mbagala Kingugi ni moja ya nyumba tano zilizoharibiwa kabisa na mafuriko hayo. Aidha nyumba nyingine 15 zimebomolewa kiasi.
Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Eng. William Mhando alilazimika kuingia kwenye lori la TANESCO na kujaribu kulitoa lori hilo lililokuwa limekwama kwenye maeneo ya Mbagala Kingugi. Lori hilo lililokuwa limebeba nguzo limekwama tangu jana. Nguzo hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya umeme iliyoharibika.
Mmoja wa wakazi walioharibikiwa na nyumba zao akimpatia maelezo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim C. Maswi jinsi nyumba yake ilivyoharibiwa.
Gari la Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) likijaribu kuvuta gari lenzake lililokwama kwenye tope wakati likipeleka nguzo za umeme kwenye eneo la Mbagala Kingungi kwa ajili ya kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko.
Mkazi wa eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam aliyejulikana kwa jina la Tyson akimpatia maelezo Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Bw. Eliakim C. Maswi juu ya uharibifu wa mali zao ikiwamo nyumba uliosababishwa na mafuriko.
Categories: Uncategorized

KIJANA DOSSANTOS ‘BABA WA MAPACHA WATATU’ ATOA SHUKRANI KWA WALIOSAIDIA KUNUSURU MAISHA YA WANAE

December 23, 2011 Leave a comment
Kijana Edwin Dossantos na mkewe waliojaliwa kupata watoto watatu mapacha mwezi wa 7 mwaka huu ametoa shukrani zake za dhati kwa wasamaria wema wote waliomsaidia kwa hali na mali kutoa michango kwa ajili ya malezi ya watoto hao kutokana na halisi ya kipato chake kuwa cha chini na maisha kuzidi kuwa magumu.

Akizungumza na Ripota Wetu alipomtembelea nyumbani kwake eneo la Kimara jijini Dar es Salaam, Dossantos amesema ni msaada wa wasamaria wema ndio umemuwezesha kumudu gharama za matumizi kwa ajili ya watoto hao haswa ukizingatia hakuwa na kazi.

Aidha Dossantos licha ya kuwashukuru wanao onekana katika orodha hii, pia amewashukuru na wale ambao hawakutaka kujulikana waliomsaidia kupitia mawakala wa M-Pesa pasipo kujitaja majina yao, ambao licha ya kuwashukuru amesema hawakumtendea haki kwa kuwa wamemnyima fursa ya kuwashukuru kwa majina yao wala namba zao.

Dossantos ametoa shukrani kwa watu waliosaidia kwa namna mbalimbali kama wanavyoonekana katika orodha ifuatayo.:-

Mr. Frank wa DSM, Mrs. Norah wa Silver Boutique, Mama Sige wa KIBAMBA, Mrs.Pamela wa USA, Mr. Sagday wa DSM, Mrs. Caroline Kazinza wa AZANIA BANK-Tegeta, Mrs. Emakulata wa UK, Miss Nyota Omary wa NORWAY, Mr. Joshua wa DSM, Mrs.Pamela wa DSM, Mrs.Mosha wa ARUSHA, Mrs. Lestituta wa DSM, Mrs. Theresia na Mrs Zahara wa Hisense DSM, Mr. Shabiby wa GAIRO Morogoro, Mrs. Fane wa DSM, Mrs. Ikupa wa AZANIA BANK-Tegeta DSM, Mrs. Vale wa AZANIA BANK-Tegeta DSM, Miss Hoyce Temu wa Channel Ten DSM, Mrs. Mercy Mariale wa DSM, Mr. Rongen Kambugu wa Kigali RWANDA, Advocate Komba wa NSSF-DSM, Miss Jehn wa DSM, Mr. Freya Mahinya wa Zanzibar, Mr. Chube wa DSM,Mr. Yusuph Mdoe wa DSM, Mr.Emmanuel Messo wa WORLD BANK-DSM, Mr. Deogratius Rweyunga wa ITV-DSM, Mr. Iddi Kibwana wa TTCL-DSM, Mr. Hashim Lundenga wa DSM na Bi. Asia Waziri Moyo wa Zanzibar.

Hata hivyo amesema watoto hao ambao kwa sasa wanaumri wa miezi 5 bado wanahitaji msaada angalau hadi wafikishe umri wa miezi 6 ambapo watakuwa wanaanza kula vyakula vya kawaida.

Katika hatua nyingine Edwin Dossantos ametoa ombi kwa msamaria mwema atakayekuwa na uwezo wa kumpatia nafasi ya kazi yoyote itakayompatia kipato cha kuweza kumudu gharama za malezi ya watoto hao.

Amesema bila ya yeye kuwa na kazi ya kumuingizia kipato anaweza kuja kwa wasamaria kuomba misaada kila mara, hivyo ameshukuru kwa kumpatia kile alichokiita samaki na sasa anaomba nyavu (Kazi) ili avue mwenyewe.

Edwin Dossantos anapatikana kwa simu ya mkononi namba 0719 909085 na 0767 646599
Categories: Uncategorized

Official Mitindo Nite mini movies, Part 1 and Part 2

December 23, 2011 Leave a comment
Categories: Uncategorized

Vodacom yatoa pole maafa Dar es salaam

December 23, 2011 Leave a comment
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mafuriko na kusababisha maafa yaliyoukumba mkoa wa Dar es salaam na kugharimu maisha ya watu kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani humo na sehemu nyingine za nchi.

Hali hii inatoa uhitaji wa taifa kushikamana na kukaa pamoja katika kuwafariji wafiwa na wale ambao walioguswa na athari za maafa hayo kwa namna moja ama nyingine.

“Tunafuatilia kwa karibu taarifa za maafa haya. Tumeguswa na vifo vya watanzania wenzetu waliopoteza maisha na tunatoa pole kwa wafiwa na tunawafariji wote waliothiriwa na maafa haya”Alisema Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.

Vodacom tayari imeshachukua hatua za awali za dharura kusaidia waathirika na itatumia shilingi Milioni 30 kutoka mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.

“Kwa sasa tunafanya mawasiliano na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambae ndie Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa kupata mahitaji muhimu ya haraka ili tuweze kutumia fedha hizo. Tunatarajia kukamilisha mchakato huu kwa haraka iwezekanavyo kutoa unafuu wa maisha kwa waathirika.”Amebainisha Mwamvita

Aidha kampuni hiyo imetangaza pia fursa kwa wateja wake kuungana na Menejimenti na wafanyakazi wake kwa kuchangia walichonacho kupitia nambari maalum ya maafa ya Vodacom Red Alert na kwa njia ya m-pesa.

Kupitia nambari ya Red Alert 15599 mteja anaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS wenye neno MAAFA na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.

“Tuna imani kuwa wote kwa pamoja tutaonesha umoja, upendo na mshikamano wetu wa kitaifa unaojenga tunu ya Utanzania wetu kusaidia wenzetu ambao kwa wakati huu wapo katika mashaka makubwa wakihitaji faraja ya kila aina”. Amesema Mwamvita.

Michango yote itakayokusanywa kupitia nambari hizi itawasilishwa kwa kamati ya Maafa ya mkoa kuongeza nguvu katika juhudi za kuwasaidia waathirika na kwamba utaratibu wa kuwapatia taarifa wachangiaji utakuwepo.

Aidha kampuni ya Vodacom Tanzania inavipongeza kipekee vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa juhudi kubwa za uokozi kwa kushirikiana na wananchi hatua ambayo bila shaka imesaidia kunusuru maisha ya maelfu ya watu.

Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa

*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.

Hatua ya 2: Chagua 4 – Lipa Bili

Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni – weka namba 155990

Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu – weka namba yako ya simu

Hatua ya 5: Weka kiasi – ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea

Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri

Hatua ya 7:Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia.
Categories: Uncategorized

Tangazo

December 23, 2011 Leave a comment
Categories: Uncategorized

BASATA: WASANII FANYENI UTAFITI KUBORESHA KAZI ZENU

December 23, 2011 Leave a comment
Mkurugenzi wa Utafiti, Mafunzo na Habari wa BASATA, Godfrey Lebejo (Katikati) akizungumza na Wadau wa Jukwaa la Sanaa wiki hii kuhusu umuhimu wa Utafiti kwenye sekta ya Sanaa. Kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Sanaa, Aristide Kwizela na Kaluona Desdery .
Mdau wa Jukwaa la Sanaa ambaye pia ni Mjumbe wa Shirikisho la Muziki, Francis Kaswahili akifafanua masuala mbalimbali kuhusu Utafiti kwenye Sekta ya Sanaa.
Wadau wa Sanaa wakifuatilia kwa makini Programu ya Jukwaa la Sanaa.

Na Mwandishi Wetu

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limeeleza kuwa, kuna kila sababu ya Wasanii kufanya utafiti wa kina kabla ya kuandaa kazi zao ili zikubalike kwa walaji na si kujifurahisha wao wenyewe.

Wito huo umetolewa wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari BASATA, Godfrey Lebejo wakati akizungumza na Wadau wa Sanaa katika ukumbi wa BASATA uliopo Ilala Bungoni kwenye program ya Jukwaa la Sanaa.

Lebejo alisema kuwa, utafiti ni muhimu pale msanii anapotafuta wazo la kuandaa kazi ili kujua itakubalika kiasi gani kwa jamii na ni ujumbe wa namna gani unakusudiwa.

“Msanii lazima afanye utafiti ili ajue mlaji wa kazi yake anataka nini. Hauwezi kutengeneza kazi ili kujifurahisha mwenyewe mwisho wa siku mlaji ni jamii inayokuzunguka” alisema Lebejo.

Aliongeza kuwa, madhara ya wasanii kutofanya utafiti husababisha kazi zao zisikubalike kwa jamii, zikose masoko, zidumu kwa muda mfupi lakini pia kuipotosha jamii kwa ujumla wake.

Aidha, aliongeza kuwa, vilio vya wasanii juu ya ukosefu wa masoko ya kazi zao, kujirudiarudia kwa kazi hizo na matatizo ya kunakili havitakwisha ikiwa wasanii hawatokuwa tayari kutumia muda wao katika kufanya utafiti.

Alisisitiza kuwa, utafiti ni moja ya mbinu za kutafuta maarifa mapya na suluhisho juu ya matatizo au changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hususani wasanii na sekta ya Sanaa kwa ujumla.
Categories: Uncategorized

TBL yakabidhi saruji kwa mkuu wa Mbeya ili kusaidia ujenzi wa shule mkoani humo

December 23, 2011 Leave a comment
Meneja wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Mbeya,Calvin Martin (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro sehemu ya mifuko ya saruji kati ya 200 yenye thamani ya sh.milioni 3,iliyotolewa na kiwanda hicho juzi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ya shule mbalimbali mkoani humo.Wa pili kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL Edith Mushi na Meneja Mauzo na Usambazi wa TBL Kanda ya Kusini, James Kavuma.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (kushoto) akitoa shukurani kwa uongozi wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) baada ya kupokea msaada huo.Kulia ni Meneja UHusiano na Mawasiliano wa TBL Edith Mushi na Meneja Mauzo na Usambaji wa TBL Kanda ya Kusini James Mavuna na Meneja wa Kiwanda cha Bia Mkoa wa Mbeya Calvin Martin.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akisalimiana na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TBL Edith Mushi mara baada ya kuwasili kukabidhiwa saruji hiyo.
M kuuwa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro (kushoto),akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) Mkoa wa Mbeya Calvin Martin mara baada ya kuwasili juzi viwanja vya Uwanja Mpya wa Ndege Songwe kwa ajili ya kukabidhiwa saruji na upandaji miti kazi iliyoratibiwa na TBL. TBL ilitoa mifuko 200 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa katika mkoa huo.
Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mbeya na wale wanaozunguka uwanja mpya wa ndege wa Songwe na wafanyakazi wa TBL walioshuhudia tukio hilo.
Categories: Uncategorized

Airtel yatoa msaada wa baskeli na cherehani kwa wakina mama wa kikundi cha UVIMA cha Mpiji Majohe

December 22, 2011 Leave a comment
Meneje huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Bi Tunu Kavisheakikabidhi moja kati ya Cherejani nne kwa Mwenyekiti chama cha UVIMA(toka shoto) Bi Tatu Ngao pamoja na Katibu wake Asha Mbelwa wa kataya Mpiji Majohe karibu na PUGU nje kidogo ya jiji la Dar es Salaamikiwa ni msaada wa Airtel kwa Vikundi hivyo vinavyohusika na kusaidiana kuwezesha jamii zenye uhitaji vilivyopo chini ya usimamizi wa Mkewa Raisi Mama Salama Kikwete. UVIMA ni Umoja wa Vikundi vilivyo chiniya WAMA. Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi za UVIMAzilizopo Majohe
Meneje huduma kwa jamii wa Airtel Tanzania Bi Tunu Kavisheakikabidhi moja kati ya Baiskeli nne kwa Mwenyekiti wa chama cha UVIMA(toka shoto) Bi Tatu Ngao pamoja na Katibu wake Asha Mbelwa wa kataya Mpiji Majohe karibu na PUGU nje kidogo ya jiji la Dar es Salaamikiwa ni msaada wa Airtel kwa Vikundi hivyo vinavyohusika na kusaidiana kuwezesha jamii zenye uhitaji vilivyopo chini ya usimamizi wa Mkewa Raisi Mama Salama Kikwete. UVIMA ni Umoja wa Vikundi vilivyo chiniya WAMA. Hafla ya makabidhiano imefanyika leo katika ofisi za UVIMAzilizopo Majohe.
Kampuni ya Simu za mkononi ya Airtel imewasaidia wakina mama wakikundi cha UVIMA cha Mpiji Majohe kilichopo PUGU nje kidogo ya jijila Dar Es Salaam kwa kuwapatia msaada wa Cherehani nne pamoja naBaiskeli nne ili zitumike kusaidia kuanzisha shule ya Ushonaji kwamanufaa ya kikundi hicho.
Wakizungumza katika hafla ya kupokea misaada ya baiskeli nne pamoja navyerehani vinne kutoka kampuni ya simu za mikononi ya Airtel wanawakewa kikundi cha UVIMA yaani Umoja wa Vikundi Vilivyo Chini ya WAMAkilichopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam katika mtaa wa MPIJIMAJOHE uliopo PUGU DSM wamesema misaada ya namna hiyo imekuwaikisaidia pia kukuza pato la Taifa.
Leo hii misaada kama hii tunayoipata inasaidia sana sisi wakina mamawa UVIMA kuweza kuzalisha chakula na hatimae tutawasaidia watotoyatima waliopo mtaani kwetu na kwenye baadhi ya nyumba za wanakikundi, pia wajane pamoja na watu wenye uhitaji maalum alisema BiTatu Ngao Mwenyekiti wa UVIMA kata ya MAJOHETunatoa ahadi kwa kampuni ya Airtel waje waone msaada waliotupatia leobaada ya miezi sita tutakuwa tumefanya mambo makubwa na mazuri zaidialiendelea kusema Bi Tatu Ngao.
Kwa upande wake meneja huduma kwa jamii wa AIRTEL, Bi. Tunu Kavisheamesema AIRTEL itaendelea kuisaidia jamii katika nyanja mbalimbaliikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ujenzi wa Taifa.
Airtel Tanzania Tulifahamu UVIMA kupitia WAMA na walitueleza jinsiUVIMA ilivyo na matarajio makubwa hivyo na sisi airtel tukaamua kutoamchango wetu huu ili kuwezesha dhamira yenu yakusaidia wajane, watuwenye virusi vya ukimwi, wazee pamoja na Watoto yatima alisema Bi TunuKavishe Meneja Huduma kwa Jamii Airtel.
Airtel bado tunaendelea na mkakati wa kuhakikisha tunasaidia jamiikupitia sehemu zote muhimu ili kupunguza matatizo ya jamii ambayo pianasisi tunaitegemea kuendelea kufanya Biashara yetuMwakani tutaendelea kujitoa katika mambo muhimu ikiwemo Elimu pamojana Afya ya jamii ili tuwe na wateja na jamii ya uhakikazaidi.alimaliza kusema Bi Tunu.
Kampuni ya simu ya Airtel imekuwa ikitoa misaada ya aina mbalimbalikatika jamii ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika huduma za jamii. 
Vikundi vya UVIMA yaani Umoja wa Vikundi Vilivyo Chini ya WAMA vikochini ya Uangaliazi wa Mama Kikwete na dhamira yake kuu ni kusaidiawakina mama, watoto yatima, jamii yenye virusi vya ukimwi, wajanepamoja na familia zenye uhitaji maalum kwa kuwapatia misaada na mbinumbalimbali za kujikwamua.
Categories: Uncategorized
Follow

Get every new post delivered to your Inbox.