Archive

Archive for November, 2011

KESI YA KINA JERRY MURO NA WENZAKE YAFUTWA NA WAO WAKO HURU SASA

November 30, 2011 Leave a comment
Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Jerry Muro na mke wake wakitoka mahakamani.
Mmoja kati ya watuhumiwa waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya shilingi milioni kumi, Edmund Kapama akitoka kwa furaha.
Mambo yoote sasa ni Dole tupu.
Pascal Kamara wakili wa Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama ya kisutu.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewaachia huru kwa mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jarry Muro na wenzake wawili.
Hakimu Frank Moshi, alisema anawaachia washitakiwa hao kwasababu upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi shaka.
Muro, Edmond Kapama pamoja na deogratius Mgasa walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba na kutaka kupokea rushwa ya Sh milioni 10 toka kwa aliyekuwa Muhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage.
Mashitaka yao yalikuwa ni ya kula njama, kuomba rushwa na kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU shitaka linalowakabili Mgasa na kapama.
Muro baada ya kutoka mahakamani alitangaza kwa wanahabari kuwasamehe wabaya wake wote ambao ni viongozi wa serikali baadhi na baadhi ya maafisa wa polisi na kuwataka waandishi wa habari kushikamana kuendelea kuibua uozo unaoendelea bila woga.
Katika hukumu, hakimu Moshi alisema baada ya kuangalia ushahidi mahakama ilikuwa na maswali ya kujiuliza kama upande wa jamuhuri uliweza kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa ambapo shitaka la kula njama kwa nia ya kuomba rushwa ambalo linawahusu washitakiwa wote, ushahidi ulikuwa wa Wage.
Shahidi huyo wa tatu wa jamuhuri lisema alikutana na Muro kwenye mgahawa wa Califonia ambapo mawasiliano kati yao yaliendelea kwa njia ya simu ya mkononi. 
Ushahidi huo ulikuwa hafifu kwasababu upande wa mashitaka haukuweza kuwasilisha karatasi ya mawasiliano kati yao kutoka kwenye kampuni ya mtandao wa simu (printout).
Vile vile alisema picha za CCTV iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa ni kivuli kisichoonyesha sura za watu badala yake wangeleta CD kuonyesha kwenye video ili watu waweze kutambulika kwa urahisi. Mawasiliano ni jambo la msingi kwasababu ili kula njama ni lazima mawasiliano yafanyike hivyo kuna mapungufu makubwa katika shitaka hilo.
Dereva aliyemwendesha wa Wage alidaiwa kuwa na Wage pale mgahawa wa Califonia walipokutana na Muro, alitakiwa kuletwa athibitishe kama Wage na Muro walikutana upande wa mashitaka hawakumwita shahidi huyo.
Katika shitaka la kuomba rushwa lilowakabili wote katika ushahidi wake Wage, alieleza Muro na wenzake walimtaka awapatie Sh milioni 10 watamsaidia kwenye tuhuma zinazomkabili lakini hakuwa nazo akawapa sh milioni moja mbali na ushahidi huo hakuna ushahidi mwingine wa serikali unaoonyesha kuwa walipokea fedha hiyo.
“Mahakama ilitegemea kuwe na ushahidi wa mawasiliano kama haupo wa kuona lakini hayo yote hayakufanyika,” alisema hakimu Moshi.
Muro alikamatwa ndani ya gari, mahakama haielewi ni kwanini kulikuwa na haraka hiyo kwanini asingeachwa wakakutana na Wage. Kwa upande wa hotel ya Sea Cliff ni sehemu ya watu yoyote anaweza kwenda.
Washitakiwa Mgasa na Kapama hakimu Moshi alisema hawakukamatwa eneo la tukio walikamatwa na kuunganishwa na halikufanyika gwaride la kuwatambua na cheti kuletwa mahakamani.
Shitaka la linalowakabili Mgasa na Kapama la kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU mahakama ilisema halikuthibitishwa lina mashaka. Alisema washitakiwa walijitambulisha kwa moja anaitwa Dr na mwingine Musa.
Upande wa mashitaka ulitakiwa kufatilia mtaani kama majina hayo washitakiwa walikuwa wakiyatumia lakini hilo halikufanyika.
“Wage kama msomi ngazi ya uhasibu aliwezaje kukubali mtu ajitambulishe kwa mdomo kama afisa wa TAKUKURU bila kuonyeshwa vitambulisho na akakubali mahakama inapata mashaka”. Aliongeza hakimu huyo hakuna vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha bila kuacha shaka hivyo wanaachiwa huru kwa mashitaka yote.
Alisema Moshi risiti, pingu na miwani havikuwa na mgogoro katika kesi na kwavile vilipatikana kwa risiti basi arudishiwe muhusika na upande unataka kukata rufaa wana ruhusiwa. Wakili kiongozi wa kesi hiyo Boniface Stanslaus alisema taafifa atampelekea Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ataamua kama watakata rufaa.
Washitakiwa walifikishwa mahakamani Februari 5 mwaka jana kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu mkazi, Gabriel Mirumbe.
Categories: Uncategorized

Mkuu wa Mkoa wa Pwani afungua mafunzo ya Afya ya Jamii Kibaha

November 30, 2011 Leave a comment
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza (kulia) akihutubia wakati wa uzinduzi wa mafunzo kwa ajili ya uanzishaji wa wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA), kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mjini Kibaha, jana. Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifa Omole.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba akizungumza wakati wa kumkarisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza mafunzo hayo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee (kushoto), akielezea umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA), wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa ajili ya uanzishaji wa wa Mfuko huo kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mkoani Pwani jana.Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifa Omole.
Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael, akijitambulisha wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha wakiwemo madiwani, wakihudhuria mafunzo hayo.
Diwani wa Kata ya Maili Moja, Kibaha, Andrew Lugano, akitoa shukrani baada ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, kufungua mafunzo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza (kulia) akiagana na Naibu Mkurugenzi wa NHIF, Hamis Mdee baada ya kufungua mafunzo kwa ajili ya uanzishaji wa wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF/TIKA), kwa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, mjini Kibaha, jana. Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Hamis Mdee na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Jenifa Omole.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Halima Kihemba, Mkurugenzi wa Hamashauri hiyo, Jenifa Omole na Naibu Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Hamis Mdee, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa halmashauri hiyo, baada ya kufungua mafunzo hayo jana.
Categories: Uncategorized

Sikinde,Msondo kupambana Krismasi TCC

November 30, 2011 Leave a comment
Sikinde Ngoma ya Ukae wakiwa kazini.
Msondo Ngoma wakiwa kazini.

Na Mwandishi Wetu

Bendi pizani za Msondo Ngoma na Mlimani Park Orchestra (Wana Sikinde Ngoma ya Ukae) zitapambana siku ya sikukuu ya Krismasi mwaka huu kwenye viwanja vya TCC Club Chang’ombe, Temeke.

Mpambano huo umeandaliwa na kampuni za Bob Entertainment na Keen Arts na kudhaminiwa na kinywaji cha Konyagi.

Mratibu wa mchuano huo Joseph Kapinga amesema pambano hilo litakuwa la funga mwaka na kuamua ni bendi gani bora kati ya magwiji hao wawili wa muziki wa dansi nchini kwa mwaka 2011.

Kapinga alisema ili kuondoa malamiko ya kuhujumiwa, hasa kwenye upangiliaji wa milio ya vyombo, kila bendi itatumia jukwaa lake kwa kupiga kwa muda wa saa moja kabla ya nyingine kupanda jukwani.

“Litakuwa pamabano la aina yake ukizingatia kuwa itakuwa ni mara ya kwanza kwa bendi hizi pinzani kupambana siku ya sikukuu ya Krismasi tangu zianzishwe” alisema Kapinga.

“Pia itakuwa ni mara ya kwanza kwao kushindana katika wilaya ya Temeke ambao ndiyo inaongoza kuwa na wapezi wao.”

Kwa kawaida Msondo Ngoma hufanya maonyesho yao kila Jumamosi kwenye viwanja vya TCC Club, Chang’ombe wakati Sikinde hufanya maonyesho yao kwenye viwanja hivyo hivyo siku ya Jumapili.

Kapinga alisema kampuni yake inafanya mipango ya kuwasafirisha wapenzi wa bendi hizo kutoka mikoa ya karibu kuja Dar es Salaam kushuhudia mpambano huo ambao pamoja na kusherehekea sikukuu ya Krismasi pia utakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 40 ya kinywaji cha Konyagi.
Categories: Uncategorized

Mtaa wa Uhuru,Kariakoo leo

November 30, 2011 Leave a comment
Nimejiuliza maswali kibao bila majibu,hivi huu uchafu hapa barabarani umefikaje??
Categories: Uncategorized

kamera ya Mtaa kwa Mtaa jijini Tanga

November 30, 2011 Leave a comment
Categories: Uncategorized

WANA RUVUMA, RUKWA NA KATAVI WAITEMBELEA MAKUMBUSHO NA NYUMBA YA UTAMADUNI DAR ES SALAAM

November 30, 2011 Leave a comment
Mkuu wa mkowa wa Rukwa Mh Eng Stella Manyanya (MB) (alie simama) akimsikiliza kwamakini Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Dkt Pual Msemwa, wengine ni wanakikundi wa Ngoma kutoka Ruvuma walio kuja kuhudhuria Tamasha la watani zao la Jamii ya watu wa  Rukwa na Katavi lililo fanyika Kijiji cha Makumbusho hivi karibuni.
Watani wa Wangoni jamii ya watu wa Rukwa na Katavi nao walipata wasaa wakuitembelea makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaama. Hapa wakiangalia magari ya Kihistoria.
Wanakikundi wa ngoma toka Mkoa wa Ruvuma wakimsikiliza kwa makini mtaalam wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni juu ya Mwenge Uliopandishwa mlima wa Kilimanjaro miaka ya 60.
Chifu Emanuel Zulu Nkosi wa Wangoni na wanakikundi cha Ngoma cha mkoa wa Ruvuma wakipata maelezo toka kwa Mama Shayo walipo tembelea makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam, Dkt Paul Mswemwa akiwakaribisha wanajamii wa Rukwa na Katavi walipo wasili makumbusho hapo.
Kikundi cha Ngoma kutoka Ruvuma kikiwa katika picha ya pamoja na Chifu wa Wangoni alie shika mtoto katikati.
Categories: Uncategorized

mchezo wa mbio za magari katika viwanja vya kawe jijini dar wafana sana

November 30, 2011 Leave a comment
 Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa katika viwanja vya Kawe,mwishoni mwa wiki ambapo kulifanyika mashindano ya mbio za magari na kuhudhuriwa na wakazi mbali mbali wa jiji la Dar.
Categories: Uncategorized

HATIMAYE TBL YAPANDISHA BENDERA YA TAIFA MLIMA KILIMANJARO

November 30, 2011 Leave a comment
Aloyce Joseph (kushoto) na Daniel Ngowi wakiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro walipoipandisha bendera ya Taifa ikiwa ni kilele cha Kampeni ya Kilimanjaro Jivunie uTanzania iliyokuwa ikiendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kusherehekea miaka 50 ya Uhuru.
Daniel Ngowi na Aloyce Joseph wakiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro walipoipandisha bendera ya Taifa ikiwa ni kilele cha Kampeni ya Kilimanjaro Jivunie uTanzania iliyokuwa ikiendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kusherekea miaka 50 ya Uhuru.
Aloyce Joseph (kushoto) na Daniel Ngowi wakiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro walipoipandisha bendera ya Taifa ikiwa ni kilele cha Kampeni ya Kilimanjaro Jivunie uTanzania iliyokuwa ikiendeshwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kusherekea miaka 50 ya Uhuru.
Categories: Uncategorized

official launch of tanzania responsible business network

November 29, 2011 Leave a comment
      Founding members of the Tanzania Responsible Business Network (TRBN) in a group photo soon after the official launch held at the Hyatt Regency, the Kilimanjaro on Monday 28th November 2011. 
     Tom Kocsis, CEO, FINCA giving introductory remarks at the official launch of the Tanzania Responsible Business Network (TRBN) held at the Hyatt Regency, the Kilimanjaro on Monday 28th November 2011.
 A cross section of guests who attended the official launch of the Tanzania Responsible Business Network.
  A cross section of guests who attended the official launch of the Tanzania Responsible Business Network (TRBN) held at the Hyatt Regency, the Kilimanjaro on Monday 28th November 2011. On the front line is Marcus Huschka , Coastal Travels (first left), Pascal Lesoinne, CEO, Twiga Cement (at the middle) and Ali Mfuruki, CEO Info Tech and Chairman of CEO Round Table (first right). Photo by Adam Mzee
Categories: Uncategorized

MAANDAMANO, FUJO NA VURUGU HAVIWEZI KUZALISHA AJIRA-CHEYO

November 29, 2011 Leave a comment
Mhe. John Cheyo akibadilishana mawazo na Bw. Oscar Fernandez-Taranco aliyewahi kuwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP) nchini Tanzania. muda mfupi kabla ya ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa wabunge kutoka mabunge mbalimbali. Bw. Taranco ambaye kwa sasa ni Msadizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akisimamia Idara ya masuala ya Siasa alikuwa miongoni mwa watoa mada.Mhe. Cheyo anahudhuria mkutano huo akiliwakilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Cheyo na Mhe. Betty Machunge wakipitia ratiba ya mkutano kati ya wabunge kutoka mabunge mbalimbali duniani na Umoja wa Mataifa, Wabunge hao walijituma vilivyo kwa kuchangia majadiliano mbalimbali yaliyofanyika katika siku ya kwanza ya mkutano huo, ambapo mada za uwajibikaji wa kisiasa, ushiriakiano kati ya Umoja wa Mataifa na Wabunge na ushiriki wa vijana katika demokrasia pamoja na mambo mengine yalijadiliwa siku ya jumatatu. Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu Asha- Rose Migiro.

Na Mwandishi Maalum

New York

Maandamano yasiyokuwa na ukomo na yasiyozingatia utawala wa sheria, vurugu na fujo zinazofanywa na vijana kwa kisingizo cha kutaka fursa sawa na uwajibikaji, hayawezi kujenga mazingira ya uzalishaji wa ajira.

Kauli hiyo imetolewa na Mhe. John M. Cheyo mbunge wa Bariadi Mashariki na mwenyekiti wa UDP, wakati alipokuwa akichangia majadiliano kuhusu fursa na changamoto za ushiriki wa vijana katika demokrasia.

Mhe. Cheyo ni kati ya wabunge wawili wanaouhudhuria mkutano wa siku mbili unaoshirikisha wabunge kutoka mabunge mbalimbali duniani, mkutano huo unafanyika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, ukiwa umeandaliwa na UN kwa kushirikiana na Chama cha Mabunge ( IPU). Mbunge mwingine kutoka Tanzania anayeshiriki mkutano huo ni Mhe. Betty Machunge

Akafafanua zaidi kwa kusema ingawa vijana wanadai uwajibikaji zaidi kutoka serikali zao pamoja na fursa za ajira, lakini ajira na fursa hizo haziwezi kupatikana katika mazingira ambayo yametawaliwa na vurugu na maandamano yasiyokuwa na kikomo.

“ Ni kweli wanayo haki ya kudai fursa sawa za kushiriki katika demokrasia na kupata ajira, lakini pia wanatakiwa kukumbuka kwamba wanaowajibu pia wa kufuata utawala wa sheria na taratibu zilizopo katika kuwasilisha madai yao, kinyume na hapo wanachokifanya si demokrasia” akasititiza Cheyo.

Akizungumzia ushiriki wa vijana katika siasa, Bw. Cheyo amesema bila ya kubadili mifumo ya uchaguzi ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya makusudi itakayoongeza idadi ya vijana mabungeni. Vijana wengi hususani Barani Afrika watabaki kuwa wasindikizaji badala ya kuwa washiriki .

Akasema kuwa vurugu nyingi na maandamano yasiyokwisha na yanayoendelea sehemu mbalimbali duniani na yakiwahusisha zaidi vijana, yanatokana na sababu nyingi lakini kubwa ni kunyimwa kwao fursa za kushiriki siasa.

“ Vijana wengi hivi sasa wamekata tamaa na wamechoka kuendelea kuwa vipandio vya watu wengine kujipatia nafasi za uongozi wa kisiasa. Kama kweli tunataka na wao washiriki kikamilifu katika siasa basi tunatakiwa kubadili mifumo yetu ya uchanguzi na hasa zile chaguzi ambazo zinatanguliza mbele fedha” akasisitiza Bw. Cheyo.

Akaongeza kuwa kila nchi inatakiwa kuweka mikakati ya makusudi itakayohakikisha kunakuwapo na ongezeko la wabunge vijana katika mabunge yao.

“ sisi katika Tanzania tumeweza kuongeza idadi ya wanawake bungeni maradufu kwa sababu tulijiweka malengo na mikakati ya kuhakikisha kwamba idadi ya wanawake inaongezeka. Kwa utaratibu huu ambao Tanzania imeutumia tunaweza pia kuutumia kwa vijana”. Akasema Cheyo.

Akizungumzia suala zima la vijana na changamoto zinazowakabili. Mhe. Cheyo ametahadharisha kwamba, vijana wasipopatiwa matumaini ni sawa na silaha ya maangamizi inayosubiri kulipuka.

Akasema wanachokifanya vijana hivi sasa katika maeneo mbalimbali duniani kama hakitaangaliwa katika umakini wake. Kuna hatari kubwa ya kujirudia kwa tabia ya kuwaondoa viongozi walioko madarakani kwa njia zisizo halali. Pamoja kurejea kwa matukio kama vile mapinduzi ya kijeshi yaliyotawala sana katika miaka ya 70 na 80.

Wachangiaji wengine waliochangia ajenda hiyo, walisema kwamba pengine vijana si wakulaumiwa sana bali wakulaumiwa ni wale wanaowatumia vijana kwa manufaa na malengo yao.

Aidha baadhi ya wachangiaji, walitaka kuwepo na tafsiri sahihi ya nani ni kijana. Kutokana na kile kilichoelezwa kwamba kumekuwa na tafrisi zinazochanganya ni umri gani unaoweza kutajwa kwamba ni umri halali wa kijana kushiriki siasa na hata uchaguzi.

“ tumezungumza sana kuhusu haki na fursa za vijana, wote tunakubaliana kwamba vijana wanahasira na wanataka mgawanyo sawa wa raslimali. Lakini hebu tuanzie humu humu katika ukumbi tuliomo, je kati yetu ni nani mbunge kijana? Hakuna. Nadhani tuna mengi ya kufanya”. Akasema mbunge mmoja kutoka Bunge la Uingereza na kuwafanya washiriki wengine kuangua kicheko.

Ajenda hiyo ambayo ilikuwa kivutio kwa wachangiaji wengi lakini pia kila mmoja akitoa maoni tofauti, na hisia tofauti katika matumizi ya vyombo vya habari vya kijamii kama vile face book na tweeter kama eneo mbadala la mawasiliano kwa vijana.

Lakini kauli za wazungumzaji wengi ilijidhirisha wazi kwamba kila aliyeichangia hakusita kusema vijana wengi si katika nchi zinazoendelea bali hata zile zilizoendelea wamechoka, wamekata tamaa na hawana matumaini ya maisha yao ya baadaye.

Naye Mhe. Betty Machunge akichangia majadiliano kuhusu dhana ya uwajibikaji, uhusiano kati ya UM na Mabunge na ushiriki wa wanawake katika siasa na demokrasia kwa ujumla. Yeye alitaka kuimarishwa na kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kati ya Umoja wa Mataifa na Mabunge.

Akasema kuwa maamuzi mengi yanayofanywa na Umoja wa Mataifa hayawafiki wabunge na kama yanawafikia basi yanachelewa mno.

Akapendekeza kuwapo na mfumo au utaratibu utakao wawezesha wabunge kupitia mabunge yao kutoa taarifa za utekelezaji wa maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa hasa yale ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi na wabunge.

Aisha akasema kuwa kama ushirikiano kati ya UM na wabunge utaratibiwa vizuri, utasaidia pia katika kubadilishana mawazo na mbinu mbadala za kuongeza idadi ya wanawake wabunge.
Categories: Uncategorized

kampuni ya Songas yakabidhi madarasa mawili ya shule ya msingi Kinyerezi leo

November 29, 2011 Leave a comment
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Ilala,Mh. Jerry Silaa akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa madarasa mawili ya shule ya msingi Kinyerezi yaliyojengwa kwa hisani ya kampuni ya Songas leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Songas bw. Christopher Ford.
Wanafunzi na walimu wa Shule ya msingi Kinyerezi wakifurahia jambo na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Ilala,Mh. Jerry Silaa na Mkurugenzi wa Songas Christopher Ford ndani ya darasa jipya lililojengwa na Songas na kukabidhiwa kwa shule ya msingi leo.
Categories: Uncategorized

Rashid Matumla VS Maneno Osward KUPIMA UKIMWI SIKU KUMI KABLA YA MPAMBANO

November 29, 2011 Leave a comment
Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ wanatarajia kupanda ulingoni kuzichapa Desemba 25 mwaka huu katika pambano lisilo la ubingwa.
Pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam .

Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema pambano hilo limeandaaliwa ili kumaliza ubishi baina ya mabondia hao ambapo katika pambano la mwisho Matumla alimchapa Oswald kwa pointi ambaye aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki wakati walishawahi kupigana mara mbili nyuma ambapo Matumla kamshinda Maneno Mara mbili na Maneno kashinda mara moja mpambano huo utakuwa wa kumaliza ubishi baina yao.

Utasindikizwa na mabondia Venas Mponji atakayezichapa na Tumaini Maguno ‘SMG’ na bondia mkongwe Rashidi Ally atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet Kalulu na Saleh Mtalekwa

Siku kumi kabla ya mpambano huo mabondia Rashidi Matumla na Maneno Osward wameshauliana kupima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi na madawa ya kuongeza nguvu kama wanatumia,sheria za mchezo huo haziruhusu kutumia dawa za aina yoyote ya kuongeza nguvu.

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo Rajabu Mhamila ‘Super D Boxing Coach’ kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

” Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd Maywhether, David Haye, Mohamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo mengi ” alisema Super D DVD hizo za mafunzo zinapatikana makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au katika kambi ya ngumi ILala na klabu ya AShanti nayo ya Ilala.
Categories: Uncategorized

WAKALA WA VIPIMO (WEIGHTS AND MEASURES AGENCY, WMA) WAPATIWA MAFUNZO YA KITAALAM KATIKA TASINIA YA VIPIMO NA MTAALAM TOKA JORDAN ENG. OSAMA MELHEM

November 29, 2011 Leave a comment
Maafisa Vipimo wakiwa katika Picha ya pamoja mara baada ya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Bi. Magdalena Chuwa (wasita tokea kushoto waliosimama mstari wa mbele) Kufungua mafunzo hayo yaliyohusu taaluma mbalimbali katika tasinia ya Vipimo kuanzia tarehe 7.Mafunzo hayo yalikuwa ni ya wiki tatu kuanzia tarehe 7-25/11/2011 yaliyofanyikia katika ukumbi wa Dar es Salaam International Conference Centre. Mambo muhimu yaliyofundishwa kwenye training hiyo ni pamoja na uhakiki wa ujazo kwa vifaa mbalimbali mfano uhakiki wa ujazo wa sindano zinazotumika katika matibabu, uhakiki wa ujazo wa chupa za maji, uhakiki kipimo kinachotumika kupimia pampu za mafuta, uhakiki wa mizani za kupimia ujazo wa bidhaa mbalimbali , uhakiki usahihi wa Thermometer (kipimajoto) n.k.
Mtaalum toka nchi ya Jordan Eng. Osama Melhem akitoa mafunzo ya jinsi ya uhakiki usahihi wa Thermometer (kipimajoto) kwa washiriki wa mafunzo toka Wakala wa Vipimo ( WMA).
Maafisa Vipimo wakifanya mazoezi ya vitendo jinsi ya kuhakiki kipimo kinachotumika kupimia pampu za mafuta
Maafisa vipimo wakihakiki ujazo wa chupa za maji.
Afisa Vipimo akihakiki usahihi wa sindano inayotumika katika matibabu.
Categories: Uncategorized

MIGIRO ATAKA WABUNGE WAWAJIBIKE KWA WANANCHI

November 29, 2011 Leave a comment
Mhe. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro akifungua mkutano wa siku mbili wa wabunge kutoka mabunge mbalimbali duniani mkutano huo unafanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, kushoto kwake ni Rais wa Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, Bw. Nassir Abdulazizi Al-Nasser na kulia ni Katibu Mkuu wa IPU Bw. Anders B. Johson.
Mhe.Naibu Katibu Mkuu Asha-Rose Migiro akibadilishana mawazo na Waheshimiwa Wabunge John M. Cheyo na Betty Machunge wakati alipowakaribisha Ofisini kwake Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.Wabunge hao wapo hapa wakihudhuria mkutano wa wabunge ambao Naibu Katibu Mkuu aliufungua. Wabunge hao wanaliwakilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo.

Na Mwandishi Maalum

New York

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Asha-Rose Migiro amewahimiza wabunge kuweka mbele maslahi ya wananchi wanaowawakilisha.

Ameyasema hayo jana Jumatatu, wakati alipokuwa akifungua mkutano wa siku mbili unaowakutanisha wabunge kutoka mabunge mbalimbali duniani, ufunguzi uliomshirikisha pia Rais wa Baraza Kuu la 66 la Umoja wa Mataifa, Nassir Abdulaziz Al-Nasser.

Katika mkutano huo ambao umeandaliwa na Umoja wa Mataifa na Muungano wa Mabunge ( IPU),Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linawakilishwa na wabunge wawili, Mhe. John M. Cheyo na Mhe. Betty Machangu.

“ Mkiwa ni wabunge kazi yenu si kupitisha sheria tu na kusimamia utendaji wa serikali. Bali mnatakiwa kuwajibika kisiasa kwa kuwasikiliza wananchi na kuelezea matakwa yao”, Akasisitiza Migiro.

Naibu Katibu Mkuu amewaambia wabunge hao, wakiwamo pia baadhi ya maspika , kwamba, uwajibikaji wa kisiasa na utawala wa kidemokrasia haviwezi kutengenishwa kwa kuwa vyote ni muhimu katika kuchagiza maendeleo ya binadamu, haki na amani.

“ uwajibikaji wa kisiasa ni muhimu sana katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili dunia hivi sasa. Baadhi ya Changamato hizo ni pamoja na umaskini, vurugu, na uhalifu wa kupangwa mambo ambayo yanashamiri katika nchi ambazo hakuna uwajibikaji” akabainisha Migiro.

Akasema kuwa taarifa ya Bank ya Dunia imeonesha kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, makosa ya jinai, vurugu na hata ugaidi na uhalifu wa kupangwa ni mambo yanayoota mizizi na kukua katika nchi ambazo ama utawala wa sheria ni dhaifu au taasisi zake zimeghubikwa na ufisadi.

Hata hivyo Migiro amewaeleza wabunge hao kwamba hakuhitajiki utafiti kama huo ulioofanywa na Bank ya Dunia,kufahamu kwamba kuongezeka kwa vitendo vya halifu kunasababishwa na serikali kandamizi.

Akatoa mfano kwa kutaja vunguvungu la kisiasa linaloendelea hivi sasa Mashariki ya Kati maarufu kama Arab Spring, ambako anasema vuguvugu hilo limeamsha hamasa hususani kwa vijana, hamasa ya kutaka kuwepo na serikali za kidemokrasia, zinazowajibika na zenye kuheshimu misingi ya haki za binadamu.

Akasema anafahamu vema changamoto wanazokabiliana nazo wabunge kwa sababu hata yeye aliwahi kuwa mbunge.

Hata hivyo akasema yapo mambo kadhaa ambayo wabunge kwa kushirikiana na serikali zao yanaweza saidia kuzuia au kupunguza mitafaruku ya kisiasa na vitendo vya  uhalifu.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na kujenga mazoea ya uwajibikaji, kufanya uchanguzi wa mara kwa mara na unaozingatia utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kukusanyika na kutoa mawazo na kuongeza idadi ya wanawake mabungeni.

“ Lakini uwajibikaji unakwenda mbali zaidi ya hapo” anasema Migiro. “ Ni kwa kuhakikisha ushiriki wa wananchi na hasa vijana katika mambo ya siku hadi siku, kwa kutimiza hayo na mambo mengine wabunge mnaweza kujenga daraja imara kati ya wananchi na serikali zao” akasisitiza Migiro.

Aidha Migiro ameyataka mabunge yote duniani yawajibike katika kuzuia vitendo vya rushwa.

Ajenda muhimu zinazojadiliwa na wabunge hao katika mkutano huo wa siku mbili ni pamoja na, uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na Mabunge , nafasi ya Umoja wa Mataifa katika kusimamia na kuimarisha dhana ya uwajibikaji, na fursa na changamoto zinazowakabili vijana katika ushiriki wao katika demokrasia.

Nyingine ni uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za umma na uimarishaji wa uhusiano kati ya taasisi za kitaifa na asasi zisizo za kuserikali ili kujenga jamii yenye uwazi.
Categories: Uncategorized

KAMPUNI YA WINLOT YAZINDULIWA NCHINI TANZANIA NAKUTANGAZA MCHEZO MPYA WA BAHATI NASIBU

November 28, 2011 1 comment
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kusimamia Michezo ya Kubahatisha nchini, Abbas Tarimba (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kampuni ya Winlot Tanzania ilivyofanikiwa kupewa leseni ya kuendesha michezo ya kubahatisha itakayoanza rasmi kuchezesha michezo hiyo hapa nchini Desemba Mosi Mwaka huu.kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Arvind Dhariyal .

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Bodi ya michezo ya bahati nasibu ya Taifa imeipatia kampuni ya Winlot Tanzania Limited.Kibali cha kuendesha bahati nasibu ya Taifa ya serikali kwa niaba ya serikali katika mchakato wa makampuni saba ya kimataifa yaliyo omba kibali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salam Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni hiyo alisema,Kampuni yake inatarajia kuzindua bahati nasibu ya taifa,ambayo wateja watatakiwa kuchagua namba na kama namba zilizochaguliwa zitafanana na namba za ushindi wateja watajipatia zawadi za pesa taslim.

Alisema hii ni fursa kwa watanzania kushiriki katika bahati nasibu tofauti ambazo zitakazowafanya kujishindia hadi kufikia zaidi ya milioni mia moja. Bahati nasibu hizi ni kama vile tiketi kuuzwa tuu baada ya mteja kuchagua namba anazopenda na baada ya kuchezechwa kwa namba alizochagua mteja zikifanana na namba za ushindi basi mteja ataweza kujishindia mpaka zaidi ya millioni mia moja.

Kampuni hiyo itachezesha michezo ya kubahatisha yenye mfumo wa draw na ile ya zawadi za papo kwa hapo, michezo hii itakuwa katika aina ya 5/90, 5/39 na 6/49. Pamoja na mifumo mingi, Winlot Tanzania itatumia pia mfumo unaojulikana kama Weaver.

 Weaver ni mfumo mahiri, wenye ubunifu mkubwa, unaotumia teknolojia mpya inaosadia pia kurahisisha michezo ya bahati nasibu kiujumla. Ni mfumo wenye umakini katika kila hatua ya michezo ya bahati nasibu.

Bwana Amani Honestus alitaja njia mbalimbali zitazo kuwa zikitumika kuchezesha bahati nasibu kuwa ni pamoja na:-

1. Tiketi tatu zitajishindia kuingia katika draw za kila siku na kila wiki.

2. Mchezo aina yaTwiga 6/49; Huu utachezeshwa kila jumamosi saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano ( 12:45pm). Zawadi ni hadi kufikia zaidi ya shilingi milioni mia moja. Mchezo huu utaonyeshwa katika televisheni.Namba za ushindi zikitangazwa, mshindia atatakiwa kwenda kuchukua zawadi zake katika ofisi za Winlot Tanzania.

3. Mchezo aina ya Duma 5/39; Mchezo huu utachezeshwa mara moja kila siku, zawadi ni hadi kufikia shilingi milioni kumi. Namba za ushindi zikitangazwa mshindi atatakiwa kwenda kuchukua zawadi zake kwa mawakala wa bahati nasibu.

4. Mchezo aina ya Simba 5/90; Mchezo huu pia utachezeshwa mara tisa kila siku, zawadi za hadi kufikia shilingi milioni mbili na nusu zitanyakuliwa.

5. Mara baada ya kutangazwa namba za ushindi,zawadi zinatakiwa kuchukuliwa katika kipindi cha siku saba. Baada ya hapo tiketi itapoteza uhalali wake.

6. Kama ilivyo katika sheria za nchi yetu, kila mshindi wa bahati nasibu atatakiwa kulipia kodi za serikali kutoka katika zawadi aliyoshinda.

7. Ili kuchukua zawadi, mshindi anatakiwa kuja na Tiketi yenye namba za ushindi.

8. Uchezeshwaji wa Draw utafanywa kila siku za Jumatatu hadi Jumamosi, saa kumi na mbili na dakika arobaini na tano (12:45pm) jioni na utashuhudiwa na mwakilishi kutoka bahati nasibu yaTaifa.

9. Tiketi zitauzwa kwa bei ndogo ya shilingi mia tano tu, hii nikutoa nafasi kwa kila mtu kuwa na uwezo wakushiriki na kujaribu bahati yake.

10. Kadri unavyonunua tiketi nyingi zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi yako ya kuibuka mshindi.

11. Mteja atatakiwa kutunza Tiketi yake mpaka mchezo utakapochezeshwa na matokeo kutangazwa.

Winlot Tanzania inasimamia miundombinu ya bahati nasibu na inabuni aina tofauti za michezo ya kubahatisha, inatoa mbinu za masoko kusaidia bidhaa za michezo ya kubahatisha, inatoa usaidizi muda wote kwa wanunuaji wa tiketi za bahati nasibu na washindi wake, na inasimamia mfumo huu wa biashara kwa ufanisi mkubwa sana.

Winlot Tanzania isingependa kubania mafanikio yake inayopata katika kusimamia michezo ya bahati nasibunabiasharanyinginezo, imejitolea kufurahia sehemu ya mafanikio haya na watu wenye uhitaji katika jamii yetu. 

Ukiachilia mbali kuwatambulisha watu wanaostahili sifa katika mafanikio yao ikiwa ni wanafunzi au raia watu wengine, Winlot Tanzania inasaidia taasisi zinazojihusisha na kazi za kujitolea katika sekta za afya, elimu nk.
Categories: Uncategorized
Follow

Get every new post delivered to your Inbox.