heri ya sikukuu ya krismas wadau woote wa Mtaa Kwa Mtaa Blog

December 25, 2011 Leave a comment
Categories: Uncategorized

Mahafali ya Saba ya Chuo kikuu cha Taifa SUZA yafanyika leo Zanzibar

December 24, 2011 Leave a comment
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA,Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wahitimu wa Mahafali ya Saba ya Chuo hicho (hawapo pichani) kabla ya kuwatunuku shahada zao katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohamed Shein,akimtunuku Shahada ya heshima ya chuo kikuu cha Taifa cha SUZA Rais Mstaafu wa
Zanzibar Dr Amani Abeid Karume,wakati wa mahafali ya 7 yaliyofanyika katika viwanja vya chuo Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,pia Mkuu wa Chuo kikuu cha Taifa SUZA Dk Ali Mohamed Shein,akimkabidhi zawadi Said Salum Bakhresa,kwa mchango wakemkubwa kukisaidia
Chuo,wakati wa mahafali ya 7 yaliyofanyika katika viwanja vya chuo Mnazi mmoja Mjini Zanzibar.
Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha SUZA,Simai Mohamed (kushoto)na Mfanya biashara maarufu Said Bakhresa na Dr Nariman Jidawi,walipompongeza kwa kupata zawadi kutokana na mchango wake mkubwa kwa SUZA,wakati wa mahafali ya 7 chuoni hapo.
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA wakisubiri kutunukiwa Shahada zao na Mkuu wa Chuo hicho ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza La Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wa katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SUZA pamoja na wahitimu wa Chuo ngazi ya Stashahada baada ya kuwatunuku Stashahada zao katika Mahafali ya Saba ya Chuo hicho yaliyofanyika leo Viwanja vya Chuoni hapo Vuga Mjini Zanzibar.picha na Ramadhan Othman IKULU ZANZIBAR.
Categories: Uncategorized

ZIARA YA MH. BENDERA , WILAYANI ULANGA , KUANGALIA UHARIBIFU WA MAZINGIRA KWENYE BONDE LA KILOMBERO

December 24, 2011 Leave a comment
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera akionesha mpaka kati ya Kijiji cha Igawa, Malinyi na Pori Tengefu la Bonde la Kilombero, ambapo wananchi wamevamia kwa kulima na kufanya malisho ya mifugo yao.
Diwani wa Kata ya Malinyi , Said Tira wa Chadema ( kulia) akieleza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera ( kati) huku Diwani mwenzake wa CCM Kata ya Igawa,Severus Kamguna, akisikiliza kwa makini
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera, (mwenye miwani) akifuata nyayo za RPC Adolfina Chialo aliyeongoza mstari, kwenda kuangalia uharibifu wa Bonde la Kilombero.
Mifugo nayo ndani ya Pori Tengefu la Bonde la Kilombero
Makazi ya jamii ya wasukuma ndani ya Pori Tengefu, Bonde la Kilombero
Gari la Polisi , Wilaya ya Ulanga, likiwa limenasa kwenye tope , ndani ya mashamba yaliyolimwa katika Bonde la Kilombero.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Igawa, Tarafa ya Malinyi, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera (hayupo pichani), wakati alipotoa amri ya kuzuia shunghuli za kilimo na ufugaji katika bonde la Kilombero.
Baadhi ya wakulima wa Wilaya ya Ulanga waliovamia bonde la Kilombero , wakirejea baada ya kupata maekelezo ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera ( hayupo pichani).
Baadhi ya wakulima na wafugaji wa jamii ya kisukuma, wakitoka mashambani ili kumsikiliza Mh. Bendera (hayupo pichani).
Sehemu ya Mashamba makubwa yaliyilimwa ndani ya Pori Tengefu katika Bonde la Kilombero, eneo la Maguba, Malinyi , Wilaya ya Ulanga.Picha na John Nditi.
Categories: Uncategorized

misaada mbalimbali yaendelea kupokelewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwasaidia waliofikwa na janga la mafuriko

December 24, 2011 Leave a comment
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (wa tatu kushoto) akipokea sehemu ya misaada iliyotolea na Umoja wa Masheikh na Wanazuoni wa Nchini Tanzania wenye jumla ya thamani ya sh. Milioni 12,kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja huo,Sheikh Hamis Mataka (mwenye kanzu nyeusi) leo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.Wengine pichani ni wajumbe wa Umoja huo wa Masheikh.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Masheikh na Wanazuoni Nchini,Sheikh Hamis Mataka (katikati) akisoma taarifa fupi ya misaada mbali mbali iliyotolewa na umoja huo kwa ajili ya waathirika wa janga la Mafuriko lililolikumba jiji la Dar es Salaam hivi karibuni wakati walipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (wa pili kulia) leo kwa ajili ya kukabidhi msaada huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq akitoa shukrani kwa wale woote waliofika ofisini kwake leo kwa lengo la kuwasilisha midaada mbalimbali kwa ajili wa waathirika wa Mafuriko yaliyotokea hivi karibu jijini Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kulia) akipokea Misaada ya vyakula kutoka kwa vijana wanaounda Muungano wa Mashirika ya Vijana nchini,Kushoto ni Kiongozi wa Muundano huo,Nyakia Ally na Katikati ni Mjumbe wa Muungano huo,Sostenes Mitti.
Kiongozi wa Muungano wa Mashirika ya Vijana nchini,Nyakia Ally (kushoto) akiongea na vyombo vya habari wakati wa kukabidhi sehemu ya misaada kwa ajili ya waathirika wa Mafuriko jijini Dar es Salaam wakati walipofika kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kulia) kukabidhi misaada yao hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadiq (kushoto) akisikiliza kwa makini taarifa ya Meneja Mauzo wa DarBrew LTD ambao ni Watengenezaji wa Kinywaji cha Chibuku,Urban Shayo wakati walipofika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kukabidhi Msaada wao kwa waathirika wa Mafuko.
Categories: Uncategorized

POLISI MKOA MJINI MAGHARIBI ZANZIBAR WATAJWA KULETA MAFANIKIO KATIKA HUDUMIA YA MWANAMKE NA MTOTO

December 23, 2011 Leave a comment
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zainzibar imesema mpango wa kuanzishwa kwa dawati linaloshughulikia kesi za kijinsia kwenye vituo vya Polisi hapa nchini kumeongeza uhuru zaidi wa kujieleza kwa watu wanaodhalilishwa na kufika Polisi kuomba huduma za kisheria.

Mkurugenzi wa Idara ya Ustawa wa Jamii, Maendeleo ya Wanawake na Watoto Zanzibar Bi. Halima Khamis, ameyasema hayo wakati alipotembelea Ofisi za Dawati la Polisi mkoa wa Mjini Mgharibi Zanzibar ambapo aliwaongoza wageni kutoka mashirika ya mbalimbali ya Kimataifa kuja kuona mafanikio yaliyopatikana katika ofisi za Dawati hilo.

Mkurugenzi huyo amesema tangu kuanzishwa kwa Dawati hilo katika mkoa wa Mjini Magharibi, Idara ya Ustawi wa Jamii Visiwani Zanzibar imekuwa ikipata ushirikiano mkubwa katika kupata ufumbuzi wa kesi za ukatili wa kijinsia.

Bi Halima amesema uwezo wa kiutendaji unaonyeshwa na Askari walipo kwenye ofisi za Dawati la Wanawake na Watoto mkoa wa Mjini Magharibi, umesaidia kuiwezesha jamii kupata huduma bora na kwa wakati jambo ambalo amesema limechangia kuamsha ari za mapambono dhidi ya matendo ya kikatili kwa wanaweke na watoto Visiwani hapa.

Amesema Ofisi hizo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wageni mbalimbali wa Kimataifa wanaotembelea Visiwani Zanzibar wakitaka kutembelea pia katika ofisi hizo kwa nia ya kujifunza zaidi.

Wakati wa Mkutano wao, Mratibu Msaidizi wa Dawati hilo Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Inspekta Fakih Yusufu Mohammed, aliwaambia wageni hao kuwa, pamoja na changamoto zilizopo, lakini Dawati hilo limepata mafanikio makubwa tangu kuanzishwa kwake mwezi Aprili mwaka jana (2010).

Inspekta Fakih amesema kuwa umuhimu wa Dawati hilo umefahamika baada ya watu mbalimbali kupatiwa huduma na elimu juu ya mapambano dhidi ya vitendo vya kikatili wa kijinsia.

Amesema hivi sasa idadi ya watu wanaofuata huduma za kisheria katika ofisi za Dawati imeongezeka kutoka watu 11 wa mwaka jana lilipoanzishwa mwaka jana hadi kufikia watu 55 mwaka huu wa 2011.

Ameyataja mafanikio mengine yaliyopatikana kuwa ni pamoja na kutoa mwamko kwa wananchi wanaopatwa na matatizo ya unyanyasaji kijinsia kujitokeza kutoa taarifa Polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe .

Amesema siku za nyuma matatizo kama hayo yalikuwa yakimalizwa katika ngazi ya familia tofauti na sasa ambapo mtazamo huo umebadilika kutokana na elimu inayotolewa juu ya madhara yatokanayo na matendo kama hayo siku za usoni.

Awali akizungumza na ujumbe huo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa bado Jeshi la Polisi linaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili wajitokeze kutoa kutoa taarofa Polisi na kwenda Mahakamani kutoa ushahidi pale wanaposhuhudia vitendo vya udhalilishwaji wa kijinsia kwa mwanamke na watoto.

Kamanda Aziz amesema kuwa matendo mengi ya kikatili yanafanywa na watu wa familia moja na hivyo kuwafanya watendewa wa makosa hayo na mashahidi kutochukua hatu kwa kuhofia kuwa wakijulikana wataweza kukamatwa na kufikishwa mahakamani na hata kufungwa jela.

Katika ziara hiyo, Bi. Halima alifuatana na wageni kutoka Shirika la Midaasa la Marekani USAID, Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Afya za Familia FHI na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.
Categories: Uncategorized

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AWATEMBELEA WANANCHI WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO DAR

December 23, 2011 Leave a comment
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya wananchi waliohifadhiwa katika Kambi ya Shule ya Sekondari ya Azania, waliookolewa katika maeneo yaliyojaa maji kutokana na mvua zilizonyesha jijini Dar es Salaam kuanzia majuzi, wakati Makamu alipofika katika Kambi hiyo leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika hao.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Bi. Monica Luis, Mkazi wa Jangwani aliyeathirika na mafuriko ya Mvua kubwa iliyonyesha jijini kuanzia majuzi, wakati makamu alipotembelea katika Kambi ya Shule ya Sekondari Azania jijini Dar es Salaam leo Desemba 23, kwa ajili ya kuwapa pole waathirika wa mafuriko hayo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wananchi waliohifadhiwa katika Klabu ya timu ya Yanga ya Jijini Dar es Salaam, wakati alipowatembelea kuwapa pole wananchi hao walioathirika na mafuriko ya Mvua kubwa zilizonyesha jijini kuanzia majuzi. Makamu alifanya ziara hiyo ya kutembelea baadhi ya kambi za waathirika leo Desemba 23.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo ya jinsi maji yalivyokuwa yamejaa wakati wa mvua kubwa iliyosababisha mafuriko, kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick (kulia), wakati alipotembelea kuwapa pole wananchi waliokuwa wamehifhadhiwa katika Klabu ya Yanga, iliyopo Jangwani leo Desemba 23. Picha na Muhidin Sufiani-OMR.
Categories: Uncategorized

VODACOM YAWAFARIJI WAATHIRIKA WA MAAFA YA DAR

December 23, 2011 Leave a comment
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadiq Meck Sadick ksuhoto akiwa na Mbunge wa Kinondoni Bw. Iddi Azan akipokea magodoro kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule .Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha Vodacom Bi. Najengwa Mbagga. Vodacom imekabidhi magodoro 430, mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani ya Shilingi 30 milioni kusaidia kambi za waathirika wa maafa ya Dar es salaam.
Sehemu ya shehena ya magodoro 430 yaliyotolewa msaada na Vodacom kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam yakiwa tayari kukabdhiwa kwa kamati ya maafa ya mkoa wa Dar es salaam. Mbali na magodoro Vodacom ilikabidhi pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.
Wafanyakazi wa Kampuni ya Vodacom wakishusha sehemu ya magodoro 430 yaliyotolewa na kampuni hiyo katika kambi ya waathirika wa maafa ya Dar es salaam ya Mchikichini. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.
Sehemu ya watoto wanaoishi katika kambi ya waathirika ya maafa ya Dar es salaam katika kambi ya shule ya msingi Mchikichini wakiwa na magodoro yaliyogawiwa na Vodacom kwa waathirika wanaoishi katika kambi hiyo. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii – Vodacom Foundation.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Bi. Beatrice Makangara kushoto na Bi. Jacqueline Tarimo wakiwaongoza wenzao kuelekea kugawa magodoro 430 yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam. Vodacom iligawa pia mablanketi 480 na vyakula vyote vikiwa na thamani shilingi 30 milioni kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation.

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom leo imekabidhi msaada wenye thamani ya shilingi 30 Milioni kwa waathirika wa maafa ya Dar es salaam wanaoishi katika makambi maalum yaliyofunguliwa kuwawezesha kujihifadhi baada ya makazi yao kuharibiwa vibaya.

Mkuu wa Mfuko wa Vodacom wa kusaidia jamii – Vodacom Foundation Bw. Yessaya Mwakifulefule amekabidhi msaada huo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambae pia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Sadik Meck Sadiq ukijumuisha magodoro 430 mablanket 800,na vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni kumi.

“Tumeshtushwa sana na hali halisi ya maafa yaliyotukumba jijini Dra es salaam, tumefika hapa kuendeleza utamaduni wa Vodacom kwa kuonesha upendo na kuwa karibu na wananchi katika nyakati za raha na shida.”Alisema Mwakifulefule.

Vodacom imekabidhi msaada huo kupitia mfuko wake wa kusaidia jamii wa Vodacom Foundation ambao umekuwa mstari wa mbele katika kusaidia juhudi za maendeleo katika jamii na pia kufariji waathirika nyakati za maafa.

“Mafuriko haya yanatajwa kuwa ni makubwa zaidi kuwahi kutokea Dar es salaam katika muda wa miaka mingi iliyopita na hivyo ni wazi athari zake ni kubwa, tunatoa pole kwa wote waliopoteza watoto, ndugu na jamaa na wale walionusurika tunawatakia afya njema na faraja katika wakati huu mgumu wa maisha wanaoupitia”Aliongeza Mwakifulefule.

Adha kampuni hiyo imetangaza pia fursa kwa wateja wake na wa wananchi kwa ujumla kuungana na Menejimenti na wafanyakazi wake kuchangia walichonacho kupitia nambari maalum ya maafa ya Vodacom Red Alert na kwa njia ya m-pesa.

Kupitia nambari ya Red Alert wananchi wanaweza kuchangia shilingi 500 kwa kutuma ujumbe mfupi – SMS wenye neno “MAAFA” kwenda nambari15599 na hakuna ukomo wa ujumbe na kwa njia ya m-pesa mteja anaweza kuchangia kuanzia shilingi 1,000 na zaidi kwenda nambari 155990.

“Mahitaji kwa wenzetu waliothirika ni makubwa. Tuna imani kuwa wote kwa pamoja tutaonesha umoja, upendo na mshikamano wetu wa kitaifa unaojenga tunu ya Utanzania wetu kusaidia wenzetu ambao kwa wakati huu wapo katika mashaka makubwa wakihitaji faraja ya kila aina”. Amesema Mwakifulefule.

Michango yote itakayokusanywa kupitia nambari hizi itawasilishwa kwa kamati ya Maafa ya mkoa kuongeza nguvu katika juhudi za kuwasaidia waathirika na kwamba utaratibu wa kuwapatia taarifa wachangiaji utakuwepo.

Aidha kampuni ya Vodacom Tanzania imevipongeza kipekee vyombo vya ulinzi na usalama nchini kwa juhudi kubwa za uokozi kwa kushirikiana na wananchi hatua ambayo imesaidia kunusuru maisha ya maelfu ya watu.

Jinsi ya kuchangia kwa m-pesa

*150*00# kupata orodha ya huduma za m-pesa.
Hatua ya 2: Chagua 4 – Lipa Bili
Hatua ya 3: Weka namba ya kampuni – weka namba 155990
Hatua ya 4: Weka namba ya kumbukumbu – weka namba yako ya simu
Hatua ya 5: Weka kiasi – ni kuanzia Tsh 1,000 na kuendelea
Hatua ya 6: Weka namba yako ya siri
Hatua ya 7:Bonyeza 1 kwa kuhakikisha muamala na tayari utakuwa umeshachangia.
Categories: Uncategorized
Follow

Get every new post delivered to your Inbox.