Home > Uncategorized > >Mjue Riyama Ally,Mcheza Filamu za Kibongo

>Mjue Riyama Ally,Mcheza Filamu za Kibongo

>

Mcheza Filamu maarufu nchini ,Riyama Ally
Nikipewa nafasi ya kuwataja waigizaji bora wa kike Bongo siwezi kusita kuanza na Riyama halafu wengine wakafuata , hii ni kutokana tu uigizaji wake ambapo anafit kila uhusika, ukimpa uchizi, umama, utoto,ukatili, upole ndo usiseme.

Riyama Ally ni msanii wa maigizo tangu mwaka 2000 wakati huo akiwa kwenye kundi la sanaa la Taswira ambaye ,anasema , hatasahau siku yake ya kwanza kuona matunda ya sanaa yake baada ya kuigiza vyema kama mtoto aliyegeuzwa kichaa na mama yake ambaye alichanganya dawa alizopewa na mganga ili ampe baba yake. Nafasi hiyo aliicheza katika tamthilia ya ‘Jabari’ iliyokuwa ikionyeshwa na kituo cha luninga cha ITV.

Riyama anasema ilipofika mwaka 2003 alijiunga na kundi la sanaa la Tamba Art Group lililokuwa likizalisha filamu za kiswahili kama ‘Miwani ya Maisha’, ‘Mzee wa Busara’ na nyinginezo nyingi ambapo yeye alicheza kwenye filamu za ‘Nsyuka’ na ‘Fungu la Kukosa’ ambazo pia ni miongoni mwa filamu zilizoandaliwa na kundi hilo.Riyama anasema mbali na filamu zinazozalishwa na kundi hilo, pia amecheza kwenye filamu nyinginezo za nje ya kundi kama ‘My Darling’ kutoka kundi la White Elephant, na akacheza pia kwenye filamu za simu ya kifo, Darkness Night, Mwana pango , Kolelo na Segito’.Kwa sasa Riyama anatarajia kuonekana tena kwenye filamu yake mwenyewe itakayoitwa ‘Mwasu’, yeye akicheza kama mhusika mkuu ambaye ataonekana kama msichana aliyelelewa katika maisha ya kitajiri lakini akajikuta akijiunga na genge la wabwia unga, madawa ya kulevya na kufanya maasi makubwa hata kuua na kupelekwa jela. 

”Hii ni baada ya wazazi wangu kuhitilafiana na kutengana hivyo mali zikasambaratika na kuwa hatuna mbele wala nyuma”, anasema Riyama.Riyama anasema pia ni mtunzi wa hadithi mbali mbali za filamu moja wapo ikiwa ni hiyo yake ya ‘Mwasu’ na nyingine ambayo ameiuzia kampuni ya CB ya Charles Mokiwa, ilioko Uingereza.

Kila la kheri Riyama sisi tunakukubali na ndio kinara wetu katika safu ya uigizaji bora hadi sasa huna mpinzani kaza buti na sio kwamba tunabisha hawa waliochaguliwa lakini habari ndio hiyooooo

Tembelea Kijiji cha FotoBara kwa Habari kemkem za namna hii
Categories: Uncategorized
  1. No comments yet.
  1. No trackbacks yet.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Follow

Get every new post delivered to your Inbox.

%d bloggers like this: